Mizzyboy

Mizzyboy

Tanzanian sensational upcoming star Mizzyboy features on Pachagazine. Mizzyboy become popular on Instagram and Tiktok after several of his videos went viral

Tanzanian sensational upcoming star Mizzyboy features on Pachagazine. Mizzyboy become popular on Instagram and Tiktok after several of his videos went viral.

Pachagazine: Tuambie kwa ufupi kuhusu Mizzyboy

Mizzyboy: Mizzy nijina la utani nililo pewa na watu, lilianza utani utani sana limepamba Moto. Mizzy nimsanii wa Kuimba na Kuigiza pia na nimpambanaji Wa hali ya chini.

Mimi Mzaliwa wa Iringa ila kwetu ni Njombe Mimi ni Mbena na kwasasa nipo Dar Es salaam Kimara

Pachagazine: Ni nini kilikuskumilia kujiunga na mziki na uigizaji

Mizzyboy: Ni kitu nacho kipenda Tangu utotoni napenda sana mziki na Uigizaji. Ni vipaji vipo ndani ya damu

Pachagazine: Umekua kwenye sanaa kwa mda gani sasa

Mizzyboy: Nimeanza Sanaa Rasmi Mwaka 2017 nimiaka kama sita Mpaka sasa

Pachagazine: Nini kimekufanya kuskuma sanaa bila kufa moyo panapo panda shuka?

Mizzyboy: Aah Uvumilivu Ndo kilakitu Na Subira za Mwenyezi Mungu Pia namuomba Mungu sana Wakati wake ndo huuu.

Pachagazine: Hivi majuzi content yako imeenea mpaka nje ya Tanzania, waweza sema nini kimechangia umaarufu wako?

Mizzyboy: Kwanza Ni MUNGU na watu pia watu ndo watazamaji na kualikana kuwa kuna jamaa anajua basi na wengine Wana pendezwa zaidi na kuposti naamini watu wamekua na mchango mkubwa kwenye huu Umaarufu wangu.

Mizzyboy_tz
Mizzyboy_tz

Pachagazine: Nini kingine unajihusisha nacho kando na sanaa?

Mizzyboy: Mimi nafanya kazi yeyote iliopo mbele yangu Sinaga ubishoo kwenye utafutaji kasoro kazi za kumkosea Mwenyezi Mungu wangu.

Pachagazine: Nyimbo zako niza cover. je kuna zile ambazo imeandika mwenyewe

Mizzyboy: Zipo Ila Na natamani kuzitoa ila Kuna mambo yako njee ya uwezo wangu. Sina pesa yakufanya Audio wala video ila nikipata boss Akataka anisaidie yeye aje tusaini mikataba tuanze kazi.

Pachagazine: Matatizo yapi umekutana nayo kama msanii kuingia kwenye industry?

Mizzyboy: Nisha Tapeliwa sana na watu wanaokuja kama wasanii pia kutuma maombi kwa mastar na yasijibiwe unatembea kwamiguu umbali mrefu alafu mafanikio hakuna. Inauma sana ilifika wakati nikakata tamaa kabisa ila bado kunamoyo ukasema Wewe bado kijana pambana nikapewa  na njia ndo hadi sasa.

Pachagazine: Umeskika kwa interview moja ukisema unamwagalia sana Diamond Plutinumz. Hivi yeye ndio role model wako?

Mizzyboy: Hapana Sina Role Model, Mimi nafanya Kwaajili ya wote pia napenda kazi za wasanii wote na nawakubali wotee kwaSababu siijui kesho yangu. Ila watu ndo huwa wanasema nafanana na Harmonize mpaka sauti.

Pachagazine: Unaweza eleza aje process ya ubunifu wako na unavyo chagua wimbo utakao igiza nao?

Mizzyboy: Sijui hata niseme nini Maana najikuta tu Nafanya Naamini Mungu pia na zinaenda sanaa

Pachagazine: Kufikia sasa kuna wasanii ambao umeigiza kupitia nyimbo zao ambao wamekutafuta?

Mizzyboy: Hapana ila napata Support kwa wtangazaji maarufu.

Pachagazine: Unaweza kushauri aje kijana anayetaka kufwata nyayo zako?

Mizzyboy: Awe mvumilivu pia apambane asisubili ashikwe mkono ndo aonywshe alicho nacho

Pachagazine: Nivideo gani unayo ipenda zaidi kwa zile ulizo achia na niipi imeenea zaidi?

Mizzyboy: Ya Harmonize Kushoto kulia

https://youtube.com/watch?v=W5MchkY54d8
Harmonize kushoto Kulia Cover Official video MIZZYBOY

Pachagazine: Mafan wako watarajie nini kutoka kwako hivi karibuni?

Mizzyboy: Kwasasa wanivumilie Wawe na subira pia Mungu akijaria watarajie kazi nzuri sitowaangusha

Pachagazine: Kwa social media watu wakupate vipi?

Mizzyboy: Watembalee Instagram na Tiktok yangu kwa jina la MIZZYBOY_TZ

Mizzyboy

:Instagram

: Tiktok

: YouTube

About Author

5 thoughts on “Mizzyboy on Pachagazine

Leave a Reply